Pangani FM

Machozi ya wajane katika jamii za wafugaji .

23 June 2021, 7:27 pm

Wakati leo Juni 23, 2021 Tanzania ikiungana na Mataifa mbalimbali kuadhimisha Siku ya Wajane Duniani, Wanawake Wajane kutoka Jamii za kifugaji Wilayani Pangani Mkoani Tanga wanaeleza changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha yao ya ujane.

Mwanamke katika Jamii hizo sio tu haruhusiwi kurithi mali pale mumewe anapofariki bali pia haruhusiwi kuolewa tena.

Mwanahabri wetu Hamisi Makungu ametuandalia taarifa maalumu ya changamoto zinzowakumba Wanawake hao.