Pangani FM

OCD Pangani atoa onyo kwa wamiliki wa majahazi.

19 February 2022, 3:50 pm

Wamiliki na manahodha wa majahazi ya mizigo wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kuzingatia sheria ya Usafirishaji kwa kuacha kubeba abiria katika vyombo vya mizigo.

Hapo jana Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Pangani Mkoani Tanga alifika katika studio za Pangani FM kuzungumzia hali ya usalama wilayani hapa ambapo aligusiapia tabia ya wamiliki wa vyombo vya usafiri baharini kusafirisha abiria kinyumena sheria.