Pangani FM

Ofisi ya Mbunge Pangani yazionya Bodi za Maji.

1 March 2021, 1:25 pm

Uongozi wa Ofisi ya Mbunge Jimbo la Pangani Mkoani Tanga umezionya Bodi za Maji Wilayani humo  juu ya swala la kusuasua kwa Miradi ya Maji kwenye maeneo yao.

Akizungumza na PANGANI FM  Mwishoni mwa wiki iliyopita moja ya viongozi waandamizi  katika Ofisi hiyo Bwana Salim KANYAMA amesema kuwa Ofisi ya Mbunge haitazivumilia Bodi za Maji kwenye hilo, na kwamba watapita kila kijiji kufuatilia utendaji wa Bodi hizo.

“Bodi za maji hizi Wenyeviti na wananchi ndio wahusika sisi Ofisi ya Mbunge tutalia nazo sana hizi Bodi sababu kuna mambo mengine yanashuka kwa Mbunge, Serikali , Halmashauri lakini Bodi ndiyo changamoto, tutakuja kusikiliza kero na tutakaa na bodi za maji, haiwezekani Mbunge wetu ni Waziri wa Maji halafu Maji Pangani yawe na shida”

Naye Katibu wa Mbunge Mwl Salimini MMARI amezitaka Bodi za Maji kuwasomea taarifa za Mapato na Matumizi wananchi na kufuata miongozo ya Serikali, ili kuepusha urasimu kwenye miradi ya MAJI.

Kwa upande wake Bwana Waziri Mbezi ambaye ni Katibu Msaidizi amezitaka BODI za Maji kushirikiana na Wananchi ambao ndio watumiaji maji ili kwa pamoja kuilinda Miradi hiyo.