Pangani FM

Mwenyekiti U.W.T awasisitiza wanawake Kugombea

6 March 2023, 9:55 pm

Mwenyekiti wa U.W.T Tanzania Bi.Mery Chatanda akionyesha tuzo maalum aliyopokea Pangani kwa niaba ya Rais wa Jamhur ya Muungano Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Bi. Mary Pius Chatanda  amewataka wanawake kuhakikisha wanachukua fomu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo.

Bi Chatanda ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya wanawake  Duniani, ambayo yamefanyika wilayani Pangani hapo Jana katika Uwanja wa Kumba.

Aidha amewataka Madiwani ikiwemo wa viti maalum kufanya ziara za Kata kwa Kata kukutana na Wanawake ili kufahamu changamoto zinazowakabili.