Pangani FM

Wazazi shirikianeni katika malezi ya watoto wenu wapate elimu bora

25 October 2023, 12:18 pm

Kutoka kulia Diwani wa kata ya Kimang’a Mhe, Salim Mwandaro mwenye kofia, katikati diwani wa kata ya Mwera Mhe, Gogo Jamhuri Mnyonge, na wa mwisho ni mjumbe wa bodi ya shule ya sekondari Funguni Bwana Hamisi Issa.( Picha na Saa Zumo)

Kila mmoja akisimama katika nafasi yake itapunguza wanafunzi kuzurura mitaani na kuacha utoro.

Na Saa Zumo.

Wazazi na walezi wameshauriwa kuwa na ushirikiano katika malezi na makuzi ya watoto ili kuwawezesha kusoma kwa bidii na kufikia malengo yao.

Hayo yamejiri katika kipindi cha Kumbe na Mimi kinachorushwa na kituo hiki ikiwa ni mjadala juu ya jitihada za wazazi na viongozi kutokomeza utoro kwa wanafunzi mashuleni.

Akizungumza kwenye mjadala huo Diwani kata ya Kimang’a Mh. Salimu Mwandaro amesema kila mmoja akisimama katika nafasi yake itapunguza wanafunzi kuzurura mitaani na kuacha utoro.

Sauti ya diwani wa kata ya Kimang’a Mhe. Mwandaro Salim.

Pili Yusuph mmoja ya wazazi akizungumza katika Mjadala huo amesema wazazi na walezi wana jukumu la kuhakikisha wana wanunulia watoto wao mahitaji muhimu.

Sauti ya Bi Pili Yusuph mzazi.

Hata hivyo Muheshimiwa Mwandaro Diwani wa Kata ya Kimang’a amesema kuwa nguvu zilizowekezwa na Serikali katika ujenzi wa Miundombinu ya elimu ni kubwa hivyo wazazi wana wajibu wa kuhakikisha Watoto wao wanasoma.