Pangani FM

Wajasiriamali waaswa kujitangaza kupitia maonesho ya Pangani.

21 September 2023, 12:10 pm

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tanga January Kilambata akizungumza kwenye maonesho ya Biashara katika Wilaya ya Pangani.

Ni nafasi pekee kwa wajasiriamali kutambulika na mabenki na fursa ya kupata mikopo.  

Na Mwandishi wetu.

Wajasiriamali wameaswa kushiriki kwenye Maonesho ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Bomani katika Wilayani Pangani ili kutangaza biashara zao.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tanga January Kilamabata ametoa ushauri huo tarehe 20/09/2023 wakati akiongea kwenye maonesho hayo ambapo amewataka Wajasiriamali kuchangamkia fursa hiyo ili kutanua wigo wa Biashara zao.

Sauti ya Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Tanga.

Amesema Benki hiyo imeendelea kuiunga mkono Serikali kwa kutengeneza mazingira mazuri ya biashara ikiwemo kutoa mikopo kwa makundi mbalimbali miongoni mwao ni Wanawake, Vijana, Wajasiliamali wadogo.

Kwa upande wao Wajasiriamali kutoka katika maeneo mbalimbali wanaoshiriki kwenye maonesho hayo wametoa maoni kuhusu mwenendo wa maonesho hayo

Sauti ya Wajasiriamali
Mjasiriamali akielezea bidhaa zake katika maonesho yanayoendelea Viwanja vya Bomani.

Maonesho hayo yanalenga kuvutia uwekezaji Wilayani Pangani katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Mifugo na Uchumi wa Buluu.