Pangani FM

Mwanaume afiriki akitafutia familia

6 June 2024, 10:43

Picha ya Bahari palipotokea ajali ya mvuvi kuzama na kufariki.

Kila mwaka katika miezi mitatu kuanzia Aprili wilaya ya Pangani imekuwa ikiandikisha ajali kadhaa za baharini zinazochukua makumi ya wakazi wa wilaya hiyo.

Na Hamisi Mkungu

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la AWESO SALIM MOHAMMED maarufu Aweso Rungo amefariki akiendelea na shughuli za uvuvi katika Bahari ya Hindi eneo la Mhembo lililopo Wilayani Pangani.

Mvuvi huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50 hadi 52 amefariki jumatano asubuhi akiwa ndani ya maji baada ya kuzidiwa na nguvu ya maji, ambapo kabla ya kufikwa na umauti alipiga kelele za kuomba msaada.

Akithibitisha tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji cha Pangani Mashariki Rajabu Kitwana Nyembo amesema tukio hilo ni la pili kutokea ndani ya mwaka huu.

Sauti ya mwenyekiti wa Pangani Mashariki Rajabu Nyembo

Akisimulia mkasa huo shuhuda wa tukio hilo Ali Abdala Mshauri amesema asubuhi wakiwa ndani ya maji kuendelea na shughuli za uvuvi, hali ya mwenzake ilibadilika hafla ambapo jitihada za kujaribu kuokoa Maisha yake zilishindikana.

Sauti ya Shuhuda

Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani Dokta Hassan Msafiri amethibitisha kupokea mwili huo majira ya asubuhi na kwamba taratibu za kuukabidhi mwili huo kwa familia zinaendelea.

Sauti ya Mganga mfawidhi hospitali ya Pangani

Mwezi wa tatu Mwaka huu mvuvi mmoja alifariki katika eneo la Muhembo wakati akiendelea na shughuli za uvuvi, kama anayoeleza Mzee Abdallah Mshauri Ramadhani mvuvi wa samaki aina ya Makaji aliyeshuhudia tukio hilo.

Sauti ya bwana Mshauri

Pangani FM inatoa pole kwa ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo. SISI NI WA MUNGU, NA KWAKE TUTAREJEA.

AMIN.