Pangani FM

Pangani kupata usafiri wa majini wa uhakika

10 October 2023, 5:48 pm

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na wananchama wa CCM katika ukumbi wa YMCA wilayani Pangani.

Fanyeni kazi mkiwa na amani, hayo mengine mlionieleza mimi ni mlezi wenu nitakwenda kuyashughulikia.

Na Saa Zumo

Halmashauri ya Pangani mkoani Tanga iko mbioni kupata uhakika wa usafiri wa majini baada ya kufanya mazungumzo na wawekezaji wa usafirishaji wa majini.

Akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Pangani katika ukumbi wa YMCA Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ndugu Hemed Suleimani Abdulla amesema mazungumzo hayo yapo katika hatua nzuri.

Sauti ya Ndugu Hemed Suleimani Abdulla

Kuhusu changamoto za miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo Ndugu Abdulla amesema atahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma.

Sauti ya Ndugu Hemed Suleiman Abdulla

Kwa upande wake mwanyekiti wa CCM mkoa wa Tanga ndugu Rajabu Abdurahman amesisitiza nidhamu kwa watumishi huku akiwaonya wanaotumia fedha za miradi ya maendeleo kinyume na makusudio.

Sauti ya Ndugu Rajab Abdurahman

Pamoja na mambo mengine Ziara ya makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar katika mkoa wa Tanga na wilaya zake imelenga kukiimarisha chama hicho kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka kesho.