Pangani FM

Hatma ya 50 kwa 50 kwa wanawake kwenye siasa ifikapo mwaka 2030

2 March 2026, 12:15

Usawa wa kijinsia ni nyenzo muhimu katika maendeleo jumuishi

Na Rajabu Mrope

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,  mwaka 2010, wagombea wanawake wa ubunge wa majimbo walikuwa 12.4 mwaka 2015 ilikuwa 2% na mwaka 2020 ni 27.6% na mwaka 2025 asilimia 32.17%.

Idadi wagombea inaonesha  mwendelezo wa ongezeko, lakini bado inaleta changamoto ya kufikia lengo la usawa wa kijinsia lililoainishwa kwenye Mkataba wa Beijing (1995) na Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ya Umoja wa Mataifa,ikizingatiwa imebaki miaka 4 kufika mwaka huo,hii inaonesha jitihada za wadau zinahitajika kwa Kipindi hiki kilichobaki na kuendelea.

Sikiliza hapa makala iliyoandaliwa na Rajabu Mrope