Pangani FM

Wakenya wengi wasusia Uchaguzi 2022.

11 August 2022, 5:25 pm

Nchini Kenya leo ni siku ya 2 tangu wananchi wake walipopanga mstari kuelekea masanduku ya kupiga kura kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi mkuu wa 2022 mara baada ya kampeni kukamilika.

Vyombo vya habari nchini humo vinajaribu kufanya hesabu za kumjua mshindi japo hesabu hizo siyo rasmi kwa maana ya kuwa si zilizothibitishwa na IEBC bali  zinatokana na picha za fomu za matokeo tu kutoka zaidi ya vituo 46 elfu vya kupigia kura.

Makamu wa Rais William Ruto na Kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakipiga kura kwa nyakati tofauti.

Suala hilo limetajwa kuchangia kuleta mkanganyiko kwa raia wa nchi hususan  katika kinyang’anyiro chenye ushindani mkali baina ya wagombea wawili wakuu, makamu wa rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Karibu kusikiliza mahojiano aliyofanya mwanahabari wetu Erick Mallya na Martin Nyoni   https://twitter.com/MartinNyoni6    Mwandishi Mtanzania aliyepiga Kambi nchini Kenya tangu kuanza kwa uchaguzi huo.

Mahojiano hayo yamejikita katika hoja mbalimbali ikiwemo  mchuano wa karibu uliopo kati ya wagombea wawili wa  nafasi ya Urais Raila Amollo Odinga wa Muungano wa Azimio la Umoja dhidi ya William Samoei Ruto wa Muungano wa Kenya Kwanza pamoja na muamko mdogo wa wakenya katika kushriki kupiga kura kwenye uchaguzi huo

 

Kuhusu Martin Nyoni 

Martin ni mwandishi wa Habari mwandamizi anayefanya kazi kama mwandishi na mhadhiri wa taaluma ya Uandishi wa Habari katika chuo cha Mtakatifu Augustino Mkoani Mwanza.