Pangani FM
Pangani FM
24 March 2026, 22:04

Wataalam wa afya katika zahanati na vituo vya afya wilayani Pangani watakuwa wakipima watu wanaohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa kifua kikuu ili waanzishiwe dawa mapema pale watakapobainika.
Na Saa Zumo
Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kifua Kikuu hii leo Machi 24, 2026, katika wilaya ya Pangani kata za Kipumbwi na Mkalamo mkoani Tanga imetajwa kuongoza kuwa na maambukizi ya kifua kikuu hali inayopelekea wilaya hiyo kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na ugonjwa huo.
Hayo yameelezwa na Abdallah Ahmed Ussi Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wilayani Pangani na kutaja makundi yanayoongoza kuwa na maambukizi hayo kuwa ni wazee na watoto.
Dkt. Ussi amewashauri wataalam wa afya katika zahanati na vituo vya afya wilayani Pangani kupima watu wanaohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa kifua kikuu ili waanzishiwe dawa mapema pale watakapobainika.
Katika mapambano dhidi ya kifua kikuu nchini Dkt. Ussi amewaomba wadau kuunga mkono wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kuwapo motisha wa kuendelea kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.
Kauli mbiu ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani 2026 ni ‘Ndiyo! Tunaweza kumaliza TB!’ kauli hii inaonesha matumaini ya kimataifa na kujitolea kwa kutokomeza kifua kikuu na inasisitiza kwamba kukomesha kifua kikuu kunawezekana kwa hatua madhubuti na ushirikiano.