Pangani FM

AKA alikuwa kama Diamond kwa Afrika Kusini

18 February 2023, 4:05 pm

Na Erick Mallya

Siku ya Ijumaa, ibada ya kumbukumbu ambayo ilikuwa wazi kwa umma ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Sandton, Johanesburg nchini Afrika Kusini katika kuadhimisha maisha ya msanii huyo na mchango wake katika tasnia ya muziki ya Afrika Kusini.

Mama mzazi wa AKA Lyne Forbes.

Mastaa wengi walipanda jukwaani, wakiwemo Dj Tira, Dj Oskido, Sizwe Dhlomo na mama mzazi wa rapa huyo, Lynn Forbes, kueleza kumbukumbu zao juu yake.

Ilikuwa mchanganyiko wa hisia kote nchini wakati ambapo maisha ya rapa huyo aliyeshinda tuzo nyingi Kiernan ‘AKA’ Forbes yakiadhimishwa katika ukumbi huo wa Sandton Convention Centre.

Mtoto wa AKA na Baba Mzazi wa Rapa huyo.

Mtangazaji wetu Erick Mallya amefanya Mahojiano na DJ Claus Mtanzania anayeishi nchini Afrika ya Kusini kujua undani wa hali ilivyo nchini humo bada ya tukio la kifo cha AKA.

Mahojiano ya Erick Mallya na Dj Mtanzania anayeishi Afrika Kusini