Pangani FM

Zaidi ya Milioni 59 kutolewa mikopo kwa vikundi Pangani.

9 November 2021, 1:17 pm

Halmashauri ya wilaya ya Pangani Mkoani Tanga imfanikiwa kutenga kiasi cha milioni 21.34 ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya halamshauri hiyo ndani ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/22 zitakazokopeshwa kwa vikundi mbalimbali vya vijana,wanawake na walemavu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Bwana Isaya Mbenje amesema kuwa fedha hizo zimeshaidhinishwa kwa ajili ya kutolewa kwa vikundi ambavyo vimewasilisha akaunti zao.