Pangani FM

Kilio cha Gwiji wa Soka Ligi Kuu Tanzania juu ya kudidimia kwa Soka la Pangani.

7 January 2021, 4:45 pm

Kufuatia mjadala uliogusa hisia za wadau wa Soka Wilayani Pangani baada ya kauli ya Kocha wa Timu ya Sakura Kids kuwa Moja ya vitu vinavyoua Soka la Pangani ni tabia ya Timu za Pangani kutumia Idadi kubwa ya Wachezaji toka nje ya Wilaya ya Pangani Leo tumefanya mahojiano na Mzee EDWARD ADEUS MWANGA maarufu kama ‘mmakonde’ mchezaji wa zamani wa timu ya NDOVU SC iliyowahi kushiriki ligi kuu soka Tanzania bara katika miaka ya 80 kipindi hiko ikiitwa ligi ya TAIFA CUP.

Mzee Edward Adeus Mwanga

Mzee Mwanga amekipiga katika klabu ya Ndovu SC na katika maisha ya Soka amecheza na magwiji kama Hamisi Gaga “Gagarino’ Mohamed Mwameja, Charles Mngolo na Lila Shomari.

Mzee Mwanga ni mzawa na mkazi wa Kimang’a hapa Wilayani Pangani. Mkali huyu wa soka wa zamani ametoa maoni yake juu ya Hoja hiyo akilinganisha na zamani ilivyokuwa na sasa.

Sikiliza hapa Mahojiano aliyofanya na Mwandishi wetu Geofrey Leonard.