Pangani FM

Barabara ya Lami Tanga-Pangani hii hapa.

1 March 2023, 1:53 pm

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi.Zainab Abdallah akiwa katika Studio za Pangani FM. Picha na Ofisi y DC

Barabara ya Tanga-Pangani KM 50, ni sehemu ya barabara ya Tanga- Pangani- Saadani -Bagamoyo  yenye urefu wa KM 256 ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Horohoro-Tanga- Pangani- Saadani – Bagamoyo  hadi Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania na Malindi-Mombasa hadi Lungalunga nchini Kenya ambayo ina lengo la kurahisisha usafirishaji wa mizigo, biashara za mipakani na kukuza utalii itakapokamilika.

Na Erick Mallya

Ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani Saadan-Bagamoyo  kwa kiwango cha lami unatarajiwa kukamilika mwezi Machi  mwaka 2025.

Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah ameyasema hayo katika majojiano maalumu aliyofanya na Pangani FM jana katika Studo za kituo hicho.

Mungu akijalia mwaka huu kipande cha Kilomita 50 utakamilika mwaka huu Tanga-Pangani Kilomita 50 inaenda kuwa na kiwango cha Lami.

Amesema Bi Zainab Abdallah

Bi Zainab Abdallah amesema ujenzi  wa awamu ya kwanza ni ujenzi wa kipande cha Kilometa 50 kutoka Pangani-Tanga ambao unatarajiwa kukamlika mwaka huu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani juu ya Ujenzi wa Barabara ya Tanga-Pangani.