Pangani FM

Aweso atembelea mradi wa Barabara ya Tanga-Pangani-Bagamoyo

6 July 2022, 5:52 pm

Mapema leo Mhe Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Hamidu Aweso amefanya ziara ya kujionea, kukagua na kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Tanga-Pangani.

Akiwa kijiji cha Choba pia amezungumza na wananchi wa eneo hilo na kuwasihi kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita kwani inayo dhamira ya dhati ya kukumilisha Mradi huu kwa wakati.

Aidha Aweso amezungumza na vyombo vya habari na  kutuma salam za Shukrani kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mwisho ameahidi kuzungumza na Waziri wa Ujenzi juu ya kumpa nguvu mkandarasi kifedha ili awe na kasi katika ufanyaji kazi kwani wananchi wa  Pangani wana kiu kubwa ya kuona barabara hiyo imekamilika.