Pangani FM

DRC kujiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki

29 March 2022, 6:04 pm

Hatimaye miezi mitatu baada ya Mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kuridhia ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kujiunga na jumuiya hiyo, baada ya kujiridhisha na kuona zipo faida za moja kwa moja za ushirikiano na taifa hilo kubwa lililo kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Machi 29 Congo DRC anakuwa mwanachama wa 7 wa Jumuiya ya Africa Mashariki

Katika hili Mwanahabari wetu Erick Mallya amezungumza na mchambuzi wa masuala ya mikakati na Diplomasia ya Kimataifa Bwana Thabit Mlangi, sikiliza hapa mahojiano hayo.