Pangani FM

Tembo ahisiwa kuua mtu Pangani

23 February 2022, 8:05 pm

Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina Shaa Omari mwenye umri wa miaka 30 amekutwa akiwa  amefariki katika eneo la Kumba Mtoni lililopo wilayani Pangai Mkoani Tanga.

Pangani FM imezungumza na kamanda wa Polisi wilaya ya Pangani bwana Cristopher Msofe ambaye amethibitisha kutokea kwa  tukio hilo.

Kamanda Msofe amedai kuwa mazingira ya ulipokutwa mwili huo yanaashiria kuwa marehemu ameuwawa na mnyama Tembo ambaye amekuwa akizunguka katika maeneo mbalimbali ya Pangani mjini.

Aidha Kamanda Msofe amedai kuwa taarifa za ndugu na wananchi waliomfahamu   marehemu huyo  zinadai kuwa alikuwa  na matatizo ya afya ya akili.