Pangani FM

Halmashauri zilizopo ndani ya mkoa wa Tanga zaagizwa kusajili vikundi vya bodaboda

8 October 2023, 2:24 pm

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Ndugu Rajabu Abrahaman

“Serikali haiwezi kuwanunulia pikipiki kama hamjajisajili kwenye vikundi”

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Ndugu Rajabu Abrahaman amezitaka Halmashauri zilizopo ndani ya mkoa wa Tanga kusajili vikundi vya bodaboda ili kuviwezesha kunufaikia na fursa mbalimbali.

Ndugu Rajabu ameyasema hayo jana akiwa katika kata ya kigombe Wilayani Muheza alipokuwa akizungumza na wananchi

Pia ameeleza namna alivyolishughulikia changamoto ya  upatikanaji wa umeme katika shule ya sekondari ya kigombe

Akiwa katika mkutano huo Naibu Waiziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo na Mbunge wa jimbo la Muheza Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma ameeleza adhma ya serikali ya kuondoka changamoto ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo.

Mbunge wa jimbo la Muheza Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma