Pangani FM

Mwili wa mtu mmoja waokotwa ukiwa umeharibika Pangani.

30 June 2022, 7:03 pm

Jeshi la Polisi Wilayani Pangani Mkoani Tanga limethibitisha kuokotwa kwa mwili wa mtu moja Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 24 hadi 25 aliyefahamika kwa jina Kombo Juma katika eneo la Kumba Mtoni lililopo kwenye kijiji cha Pangani Magharibi Wilayani humo.

 

Leo mchana majira ya saa 7 Mkuu wa upelelezi wilaya ya Pangani ASP Adam ameambatana na Mwenyekiti wa kijiji cha Pangani Magharibi pamoja na Diwani wa Kata ya Pangani Magharibi katika eneo la tukio baada ya kupata taaarifa kutoka kwa Wananchi.

 

Wananchi hao wamedai kuuona mwili huo baada ya kusikia harufu kali katika maeneo hayo ambapo baada ya kufuatilia ndipo walipouona mwili huo

 

Pangani FM imezungumza pia na Mwenyekiti wa kijiji cha Pangani Magharibi Bwana Oska Albert akiwa katika eneo la tukio ambapo pamoja na kuthibitisha taarifa mbalimbali za mwili huo ameowaomba wananchi kutohofia kutoa ushahidi pale yanapotokea matukio kama hayo

 

“Mnamo saa 5 nikiwa Ofisini kwangu alikuja mtu akaniambia kule dampo kuna maiti haitambuliki nilianza kutafuta Uongozi wa juu tukatoa taarifa Polisi tukaelekea eneo la tukio lakini baada ya kufika pale katika kumuangalia na uhalisia aliokuwa nao na nguo alizofaa , pamoja na Begi tumemkuta ana Begi, Panga tumemtambua kwamba anaitwa Kombo Juma kwa hiyo taratibu zote za kisheria zimeendelea na kuzika mwili wa marehemu, umri wake anakaribia miaka 24-25 sababu hatujaijua vizuri sababu alikuwa na matatizo ya akili na alikuwa anafanya kazi zake kwenye maeneo tuliyomkuta alikuwa anagongagonga kokoto mpaka sasa sababu hatujajua kifo chake kimetokana na nini”- Amesema Mwenyekiti Pangani Magharibi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo mwili huo umekutwa maeneo ambayo ni rahisi kwa watu kuuona ila kutokana na hofu ya kutoa taarifa Polisi ilipeekea Wananchi kukaa kimya hivyo kupelekea  mwili huo kuharibika zaidi.