Elimu yahitajika kukomesha unyanyapaa kwa wagonjwa wa afya ya akili
10 October 2023, 2:50 pm
“Magonjwa ya afya ya akili yanatibika iwapo utabaini mapema na kuanza matibabu“
Na Mwandishi wetu
Kukosekana kwa elimu ya kutosha kwenye jamii juu ya magonjwa ya afya ya akili kumechangia unyanyapaa kwa watu wanaougua magonjwa hayo.
Hayo yamesemwa na mwanasaikologia Anastazia Nturu kutoka kituo cha Nobal Health kilichopo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na Pangani FM kupitia kipindi cha Asubuhi ya leo ikiwa dunia inaadhimisha siku ya afya ya akili.
Amezitajia dalili za ugonjwa ikiwa ni pamoja na mtu kushindwa kutekeleza majumu yake ipasavyo na kuonesha hali ya wasiwasi
Sauti ya Anastazia Nturu
Kwa upande wake mwanasaikolijia Alpha Kipanga kutoka kituo cha Nobal Health ameishauri jamii kuwa makini katika kutambua mabadiliko ya mtu mmoja mmoja na kubaini kama mtu ameathiriwa na ugonjwa huo ili aweze kupata matibabu mapema kwani ugonjwa huo unatibika katika hatua za awali.