Pangani FM

Wiki ya AZAKI 2021

1 November 2021, 2:04 pm

Wiki ya AZAKi 2021 ilianza tarehe 23 hadi 28 Oktoba katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre mjini Dodoma.

Tukio hili ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya Asasi za Kiraia nchini Tanzania.

Tukio hili linalenga kuwaleta pamoja wanachama wakuu wa Asasi za Kiraia na washikadau wao ili kushiriki katika majadiliano ya kina juu ya kazi zao, kubadilishana uzoefu, na kuona jinsi AZAKi zinaweza kushirikiana kimkakati na wananchi, serikali, wafadhili, na sekta binafsi.

Tukio hilo lilianza kwa siku mbili za maonyesho yanayoshirikisha AZAKi za ndani na kimataifa na mkutano wa siku nne.

Wiki ya Asasi za Kiraia ilianza kwa maonyesho ya wasanii wa hapa nchini na kufunguliwa rasmi na Spika wa Bunge Job Ndugai.

Tukio la mwaka huu lilikuwa la tatu katika mfululizo maadhimihso hayo

Zaidi ya AZAKi 1500 zilishiriki zikiwemo za ndani na za Kitaifa zenye wawakilishi kutoka balozi, wafadhili, wabunge, mawaziri, viongozi wa Serikali na wadau wengine wenye nia kama hiyo.

kauli mbiu ya Wiki ya Azaki 2021 ilikuwa ni ‘Mchango wa Azaki zisizokuwa za kiserikali katika maendeleo ya Taifa’

Mwandishi wa Habari na Afisa Programu wa Shirika la UZIKWASA Bw. Erick Mallya akizungumza na Mkurugenzi wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga wakati wa maadhimisho ya CSO Week 2021.

Sikiliza hapa mahojiano ambayo amefanya mwandishi wetu Erick Mallya na Mkurugenzi wa FCO bwana Francis Kiwanga.