Pangani FM

Wadau wa sekta ya uvuvi Pangani watakiwa kushirikiana kulinda rasilimali za bahari

9 October 2023, 2:36 pm

Wadau wa Sekta ya Uvuvi wakichangia mada kupitia kipindi cha “Nitunze Nikutunze”

“Tungekuwa tumepata elimu mapema, tungejua wa kulia nae”

Na Abdilhalim Shukran

Wataalamu wa sekta ya Uvivi wilayani Pangani wametakiwa  kushirikiana na wavuvi kuimarisha jitihada za kulinda rasilimali za bahari.

Ushauri huo umetolewa na wadau wa sekta ya uvuvi katika wilaya ya Pangani wakati wakichangia mada kupitia kipindi cha “Nitunze Nikutunze” kinachorushwa na kituo cha redio cha Pangani Fm.

Sauti ya wavuvi wakichangia mada

Katika hatua nyingine wadau hao wamesema suala la kulinda na Uvuvi haramu unavyofanywa na baadhi ya wavuvi unachangiwa na kukosekana kwa ushirikiano kati ya wavuvi na wataalamu wa sekta hiyo

Kwa upande wake Afisa Uvuvi Wilaya Pangani JOEL MABAGALA amehidi kuzifanyia kazi changamoto zilizotolewa na wavuvi hao huku akiwasihi kufata sheria na taratibu za uvuvi kama zilivyo Pangwa.

Sauti ya Afisa Uvuvi (W) ya Pangani Joel Mabagala

Pamoja na kuhidi kuyafanyia kazi mapendeko ya wavuvi Bwana JOEL amewataka wavuvi kujiunga katika vyama vya uvuvi na ushirika ili waweze kupata fursa zinazotolewa na serikali na wadau wengine wa  sekta ya hiyo.

Sauti ya Afisa Uvuvi (W) ya Pangani Joel Mabagala