Pangani FM

MIA za Rais Samia Pangani-Barabara

29 June 2021, 11:42 am

Wakala wa huduma za barabara mjini na vijijini TARURA Wilayani Pangani Mkoani Tanga wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kufikisha Siku 100 Madarakani tangu aapishwe kuwa Rais wa awamu ya Sita JMT

TARURA Pangani wamesema katika Siku 100 za Rais Samia Madarakani, amefanikiwa pia kuongeza Fedha za Miradi ya Barabara.

Hayo yamezungumzwa na meneja wa TARURA wilayani humo Enjiania Eliya Mgaya wakati wa mahojiano maalum na kituo hiki ofisini kwake kuhusu siku 100 za kiongozi huyo tangu alipoapishwa Machi 19 Mwaka huu. 

sikiliza hapa taarifa iliyoandaliwa na mwanahabari wetu Mtumwa Kombora