Pangani FM

Zainab Abdallah awaaga Wananchi wa Pangani.

23 June 2021, 4:25 pm

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah Issa ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, amewaaga rasmi wananchi na viongozi wa Pangani, pamoja na wadau Wilayani humo kupitia kituo cha Pangani FM.

Bi Zainab Abdallah akiwa katika Studio za Pangani FM

Akizungumza kupitia Pangani FM Bi.Zainab amewashukuru wananchi wa Pangani kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote cha uongozi wake, pia ameaomba wananchi kumpa ushirikiano Mkuu wa Wilaya mpya wa Panani Bwana Ghaibu Buller Lingo .

“niwashukuru wadau wote wa maendeleo na hasa wenzangu wa UZIKWASA mmekuwa mkinipa ushirikiano sana toka siku ya kwanza mpake leo naondoka na mimi kama mwenzenu nimeona si busara kuondoka kimyakimya nilitamani kupitia kila kata niage lakini kwa nature ya kazi zetu Mama anasema zege halilali, nimeona ni busara nikaongea na Wananchi Kuptitia Pangani FM naamini ndio fursa pekee ambayo naweza kuwasiliana na wananchi wote wakanisikia, naahidi ushirikiano sababu Bagamoyo na Pangani ni majirani, naombeni mumpe Ushirikiano mkuu wa wilaya mpya ili kusukuma maendeleo ya Pangani” – Amesema Bi Zainab Abdallah

Ghaibu Lingo anakuwa mkuu wa wilaya ya Pangani wa 22 akipokea nafasi hiyo kutoka kwa  Zainabu Abdallah Isa ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Sikiliza hapa mahojiano hayo