Pangani FM

Angalizo la Upepo Mkali lawafikia wavuvi Pangani.

5 March 2021, 9:38 pm

Kufuatia Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA hapo jana kutoa angalizo la uwepo wa vipindi vya upepo mkali unaofikia kilimita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia ukubwa wa mita 200 kuanzia tarehe 4 hadi 8 mwezi wa 3 -2021, wavuvi mjini Pangani wameelezea namna wanavyochukua hatua baada ya taarifa hiyo.

ANGALIZO hilo la TMA limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi (Mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (Ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Mwandishi wetu COSMAS CLEMENT amewafikia baadhi ya wavuvi katika ufukwe wa bahari ya hindi hapa Pangani mjini na kuandaa taarifa ifuatayo.