Pangani FM

TANGA UWASA Kufufua Visima vya Maji Pangani.

2 March 2021, 11:19 am

Mamlaka ya usimamizi wa Maji  Wilayani Pangani kupitia TANGA UWASA imejipanga katika uboreshaji wa miundombinu ya umeme ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji wilayani hapa.

Hayo yameelezwa na Meneja wa maji TANGA UWASA Ndugu JOHN FUSSI wakati akizungumza na PANGANI FM  ambapo ameeleza kuwa changamoto wanazokutana nazo katika utoaji wa huduma kwa wateja wao ni pamoja na wateja kutopata maji ya kutosha.

‘’changamoto ambazo tumezikuta katika huduma ya maji pangani ni kwamba wateja wetu hawapati maji ya kutosha, miundombinu tuliyoikuta ina mabomba chakavu kiasi kwamba yanavujisha maji mengi na changamoto ya tatu ni mitambo kuchoka na kusababisha kila wiki tuwe na marekebisho ya mara kwa mara na changamoto nyingine ni mabomba yaliyolazwa hayapo katika hali ya mpangilio unaotakiwa, na mwisho ni wateja wengi hawajafungiwa mita kwa hiyo ni vugumu kuwahesabia matumizi ya maji yaliyotumika na kuna suala la nishati ya umeme kuwa tatizo hii inatukwamisha katika uendeshaji wa mitambo.’’

Amesema FUSSI

Aidha FUSSI amesema kuwa mikakati iliyopo kwa mwaka huu wa 2021 ni kufufua visima vya maji ili kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya watumiaji wa maji na kuhakikisha kila mteja anapata huduma yenye uhakika.

Kwa sasa mikakati yetu ni umeme kwa hiyo kuanzia mwezi huu hadi mei tumejipanga kuwa na ‘Transformer’ yetu wenyewe ambayo haitaishiwa nguvu tena katika usukumaji wa maji, mpango mwingine ni kufufua kisima ili kuongeza uwezo wa maji, tuna kisima kimoja tutakachokifufua na tuna kisima kipya hiki tutakifunga pump mpya yenye uwezo wa kusukuma maji, na matarajio yetu ni kukidhi huduma hii kwa wateja wetu kwa kiwango kikubwa

Amesema Bwana Fussi.

Aidha amewataka wakazi wa Wilaya ya Pangani kutoa ushirikiano pale wanapokutana na uvujifu wa maji katika miundombinu ili mamlaka iweze kuchukuwa hatua.