Pangani FM

Pangani FM yaibuka kidedea tuzo za EJAT 2020.

13 September 2021, 9:34 am

Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Radio Pangani FM Rajabu Mustapha Mrope  ameibuka  mshindi wa kwanza Kitaifa wa tuzo za umahiri wa Habari Tanzania (EJAT) mwaka 2020 katika kipengele cha Habari za Data na Takwimu.

Makala iliyopelekea ushindi huo ilionyesha namna ambavyo wapiga kura walipungua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulinganisha na miaka mitano iliyopita.

Juma ya kazi 147 ziliwasilishwa kwa Baraza la Habari la Habari Tanzania ili kushindanishwa katika kinyang’anyiro hicho.

Tuzo hizo zimetolewa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na waandishi wachache huku sehemu kubwa wakishiriki kupitia njia ya Mtandao kama tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza mara baada ya kutajwa kama mshindi katika tuzo hizo Bwana Rajabu Mrope amelishukuru Shirika la UZIKWASA kwa uwepo wake kwenye Safari Yake ya uandishiwa Habari pamoja na timu nzima ya waandishi wa kituo hiki katika kufanikisha ushindi wake.

Mwandishi wa Habari wa Pangani FM Rajabu Mustapha Mrope

Hii ni mara ya Pili mfululizo kwa Rajabu Mrope kuibuka mshindi katika tuzo hizo na mara ya sita  mfululizo kwa Pangani FM kutoa mshindi katika Tuzo hizo kubwa Zaidi za Habari nchini Tanzania.