Pangani FM

Pangani watakiwa kufanyia kazi taarifa za majanga ya asili

15 October 2023, 1:32 pm

Picha kwa hisani ya mitandao

“Ni vyema wananchi wakachukua tahadhari wanapoona viashiria vya majanga na pia kuepuka kujenga nyumba kiholela.”

Na Catheline Sekibaha

Wananchi wilayani Pangani mkoani Tanga wametakiwa kuchukua tahadhari wanapopewa taarifa za uwepo wa viashiria vya matukio ya majanga ya asili ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Wito huo umetolewa na Afisa Mazingiura wilaya ya Panganni Daudi Mlahagwa wakati akizungumza na Pangani FM ambapo amesema ni vyema wananchi wakaepuka kujenga nyumba kiholela.

Sauti ya Afisa Mazingira (W) Pangani Daud Mlahagwa

Aidha afisa mazingira amesema wakati mwingine majanga ya asili  yanapelekea vitendo vya ukatili kwenye familia kutokana na aina ya na utafutaji wa riziki kwa njia ambazo zinachangia ukatili zaidi

Sauti ya Afisa Mazingira (W) Pangani Daud Mlahagwa

Hayo yamekuja kufuatika siku ya Kimataifa ya kupunguza hatari ya majanga ya asili ambayo huadhimishwa kila Okt 13 ambapo mwaka huu siku hii imeadhimishwa kwa jamii kuhimizwa kushughulikia uhusiano kati ya majanga na ukosefu wa usawa