Pangani FM

Wito: Wenza jadilianeni pamoja kuimarisha mahusiano

12 October 2023, 4:00 pm

Wenza wametakiwa kuzungumza kwa pamoja changamoto wanazokutana nazo kwenye mahusiano ili waweze kupata msaada wa kutatua changamoto hizo.

Na Mariam Ally

Wakiongea na kituo hiki kupitia kipindi cha Busati la wenza wawezeshaji ngazi ya jamii kutoka katika kijiji cha Mwera na Ushongo wilaya ya Pangani mkoani Tanga, wamekiri uwepo wa matukio ya ukatili kwa wanaume ndani ya ndoa.

Wawezeshaji hao Chausiku John kutoka kijiji cha Mwera na Mwasiti Fahamuni kutoka kijiji cha Ushongo wamesema tabia ya baadhi ya wanandoa kukaa kimya wanapokutana na changamoto mbalimbali kwenye ndoa zao imekuwa ni kikwazo katika kutatua changamoto hizo.

Sauti za Wawezeshaji

Wameongeza kuwa kwa sasa matukio ya ukatili yamepungua huku wakisema elimu iliyotolewa na shirika la UZIKWASA kwa wawezeshaji hao imewafanya wanandoa kutambua namna ya kutatua kesi zinazohusiana na matukio hayo.

Sauti za Wawezeshaji

Shirika la UZIKWASA lililopo Boza katika wilaya ya Pangani mkoani Tanga limeendelea kuwezesha mafunzo katika ngazi ya jamii kwa lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya  matukio ya ukatili kwenye maeneo ya wilaya hiyo.