Pangani FM

Miradi 9 kumulikwa na mwenge wa uhuru Pangani

19 May 2023, 2:57 pm

Na Saa Zumo

Miradi tisa ya kimaendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8 inatarajiwa kukaguliwa katika mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2023 wilayani Pangani mkoani Tanga.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya mapokezi ya mwenge wilayani Pangani mwaka huu  mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah  amesema kuwa mwenge wa uhuru unatarajiwa kupokelewa wilayani Pangani  Juni 10 mwaka huu.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Bomani uliopo wilayani Pangani mkoani Tanga na kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Pangani wakiwemo madiwani, watendaji kata na watendaji wa vijiji.

’Tutaupokea mwenge wa uhuru katika kijiji cha Kimang’a ukitokea Tanga mjini na sisi tutaukabidhi kwa wilaya ya Muheza’’ .

Amesema Bi. Zainab Abdallah

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani katika kikao hicho

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewaagiza viongozi mbalimbali wa walaya ya Pangani kufanya  hamasa katika maeneo yao ili wananchi wajitokeze kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge.

Kikao kama hicho kitakaliwa tena tarehe 2/6/2023, Mwenge huo unatarajiwa kukesha katika viwanja vya Kumba mjini Pangani.