Pangani FM

UZIKWASA kuboresha usikivu Pangani FM

27 April 2024, 1:09 pm

Mkuu wa (W) Pangani Mussa Kilakala akiwa kwenye picha ya Pamoja na viongozi wa dini na wafanyakazi wa UZIKWASA.

UZIKWASA imeanza kufanya maboresho ya usikivu wa redio Pangani FM kufuatia athari za mvua zinazoendelea kunyesha.

Na Hamisi Makungu

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Tanga zimechangia kuathiri mitambo ya Kituo cha Radio Pangani FM iliyopo Mkanyageni wilayani Muheza.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) Bwana Novatus Urassa katika hafla ya ufunguzi wa jengo la Kituo cha Radio Pangani.

Bwana Urassa amesema hali hiyo imepelekea kukosekana kwa usikivu katika baadhi ya maeneo ambayo ilikuwa ikisikika vizuri.

Sauti ya mkurugenzi wa UZIKWASA Bwana Novatus Urassa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Musa Kilakala aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo mbali na kulipongeza shirika hilo amehimiza ushirikiano katika kuisaidia jamii ya Pangani na taifa kwa ujumla.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Pangani Mussa Kilakala.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) Bwana Nyantito Machota pamoja na mambo mengine amesema uungwaji mkono wa shughuli zinazofanywa na Shirika ndio chachu ya mafanikio yanayoshuhudiwa.

Hafla hiyo iliyojumuisha wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Kata ya Kimang’a, Viongozi wa Dini, na majirani ambapo awali jengo hilo lilizinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa April 16 Mwaka huu.