Pangani FM

Simanzi: Binti aliyejinyonga Pangani

11 April 2023, 11:05 am

Binti mmoja anayefahamika kwa jina la Mwajuma Fadhili anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14 mwanafunzi wa Darasa la Saba wa shule ya Msingi Kimang’a wilayani pangani Mkoani Tanga amekutwa amejinyonga Aprili 9 usiku.

Akizungumza na Pangani FM kaimu mkuu wa polisi wilaya ya Pangani SP Fatuma Joseph amesema tukio hilo limetokea tarehe 9 majira saa Mbili na nusu usiku ambapo  binti huyo alijinyonga kwa kutumia Kamba ya chandarua iliyosokotwa ndani ya nyumba yao na jeshi la polisi linaendelea kuchunguza sababu ya tukio hilo.

Pangani FM ilizungumza pia na  mwenyekiti wa Kijiji cha Kimang’a Edna Makenya ambaye  alithibitisha kuwa alipata taarifa ya uwepo wa tukio hilo na kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi.

Mwili wa Binti huyo umeshazikwa katika wilaya ya Tanga kata ya Pongwe.

Pangani FM inatoa Pole kwa Familia iliyopatwa na msiba huo.