Pangani FM

Wazazi waaswa kuwalinda wanafunzi kipindi cha likizo

13 December 2023, 11:03 am

Mwalimu Godlisten Mbowe akiwa katika kipindi cha Redio darasa

Matukio mengi ya ukatili kwa wanafunzi hutokea kipindi cha likizo hivyo wazazi wawe makini kuwalinda watoto wao.

Na Cosmas Clement.

Wazazi na walezi wa wanafunzi wilayani Pangani mkoani Tanga wameaswa kuwa makini na kuimarisha usimamizi kwa watoto wao katika kipindi hiki cha likizo ili kuwaepusha matukio yatakayohatarisha ndoto zao kielimu.

Hayo yamezungumzwa na mwalimu Herieth Muhina na Mwalimu Godlisten Mbowe katika kipindi cha redio darasa kinachorushwa na redio pangani fm.

Wamesema wazazi wanapaswa kuimarisha ulinzi na ufuatiliaji kwani katika kipindi hiki cha likizo kumekuwa na matukio mengi ya hatari kwa watoto.

Mwalimu Godlisten Mbowe na Mwalimu Herieth Muhina

Wamewaasa wanafunzi kutumia kipindi cha redio darasa kinachorushwa na kituo cha redio pangani FM ili kuendelea kujifunza masomo yao wakati huu wa likizo.

Mwalimu Godlisten Mbowe na Mwalimu Herieth Muhina

Kipindi cha redio darasa kwa kawaida hurushwa siku za jumamosi na jumapili huku kipindi cha likizo kikirushwa kila siku jumatatu mpaka jumapili ili kuwapa fursa wanafunzi kujifunza masomo ya darasani wakiwa nyumbani.