Pangani FM

Hatua zaanza dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wanawake Pangani

15 February 2023, 4:55 pm

Picha na Erick Mallya

Na Erick Mallya

Wadau mbalimbali wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kuogeza jitihada zao katika utunzaji wa mazingira na kuiwezesha jamii kushiriki kikamilifu katika kuzuia na kustahimili mabadiliko ya tabia nchi ili kuwanusuru wanawake dhidi ya masaibu mbalimbali wanayokutana nayo ambayo ni matokeo ya athari za mabadliko ya tabianchi.

Hayo yamejiri katika mafunzo ya siku nne ya kuijengea uwezo kamati ya mazingira ya kijiji cha Kwakibuyu wilayani Pangani Mkoani Tanga katika kuhusisha masuala ya jinsia kwenye mipango kazi yao. Mafunzo yaliyotolewa na shirika la UZIKWASA kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Pangani.

Sikiliza hapa juu ya hatua zinazochukuliwa na shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kwakibuyu wakishiriki mafunzo hayo.