Pangani FM

Shule za Pangani zafanya vizuri matokeo ya kidato cha Sita 2022.

6 July 2022, 5:10 pm

 

Baraza la mitihani nchini NECTA hapo jana limetangaza matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2022.

Matokeo hayo yamezionyesha shule za wilaya ya Pangani kufanya vizuri.

Jumanne Julai 5 Mbunge wa Jimbo la Pangani Mh. Jumaa Hamidu Aweso amefanya kikao na maalum kilichowakutanisha wazee mbalimbali wa wilaya ya Pangani ambapo katika kikao hicho katibu tawala wa wilaya ya Pangani Bw. Hassan Nyange alitumia nafasi hiyo kutoa mchanganuo wa ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha sitatoka shule za Pangani.

Nyange amesema kuwa katika shule ya Sekondari ya Mwera iliyokuwa na wanafunzi 57 wanafunzi 17 wamepata daraja  1, wanafunzi 38 wamepata daraja 2 wanafunzi wawili wamepata daraja 3 na hakuna Divisheni 3 wala 4.

Katika shule ya Sekondari ya Sayansi ya Tongani iliyopo katika kijiji cha Mkalamo wilayani humo yenye michepuo ya CBG na PCB wanafunzi wawili wamepata divisheni 1, wanafuzi 19 wamepata daraja 2, wanafunzi 27 wamepata daraja 3 na wanafunzi wawili wamepata daraja 4.

Kufuatia matokeo hayo Mbunge wa Jimbo la Pangani ambaye pia ni waziri wa maji nchini Mh. Jumaa Hamidu Aweso ametoa pongezi kwa wanafunzi , walimu , wazazi na wadau wote wa elimu Pangani pamoja na kuwasisitiza wazazi kutoa ushirikiano kwa walimu ili ku

 

“Haya ni mafanikio mazuri sana kwa elimu Pangani, tuendelee kushirikiana kuhakikisha suala la elimu linakuwa vizuri katika jimbo letu la Pangani na niwaombe Wananchi wa jimbo la Pangani walimu wetu wanafanya vizuri sana wanastahili kuungwa mkono lazima tushirkiane nao katika kuhakikisha wadogo zetu wanafanya vizuri na wanaendelea kufaulu ili waje kuisaidia jamii ya Pangani na kulisaidia taifa letu la Tanzania”Amesema Mh. Aweso