Pangani FM

Jinsi msimu wa uvuvi unavyosaidia kupunguza matukio ya wizi Pangani

13 December 2023, 11:26 am

Mfanyabiashara na mchakataji wa dagaa akiendelea na harakati za uandaaji wa dagaa uono katika ufukwe wa bahari ya hindi pangani Mjini.

Katika msimu wa uvuvi naweza kupata hata shilingi laki tatu kwa siku kwa kuuza dagaa, pia changamoto ya vijana kuiba yamepungua.

Na Cosmas Clement.

Kuanza kwa msimu wa uvuvi wa dagaa katika mji wa Pangani kumetajwa kuwa ni fursa nzuri kwa wakazi wa mji huo katika kuwawezesha kujipatia kipato cha siku.

Msimu huo wa uvuvi unaoanza mwezi wa tisa mpaka mwezi wa nne huwawezesha wavuvi kuendesha shughuli za uvuvi wa samaki aina mbalimbali ikiwemo dagaa uono katika bahari ya hindi mjini Pangani kwa urahisi tofauti na miezi mingine.

Wakizungumza na Pangani FM baadhi ya wanajamii wilayani Pangani wamesema tangu kuanza kwa msimu huo wa uvuvi wamekuwa wakiingiza kipato kizuri cha siku na kusaidia familia zao.

Sauti za wakazi wa Mji wa Pangani

Pamoja na kuongeza kipato, wakazi hao wamesema msimu wa uvuvi umesaidia kupunguza changamoto za wizi kwa kuwa vijana wanapata chanzo cha mapato.

Sauti ya wakazi wa mji wa Pangani

Shughuli ya uvuvi ni miongoni mwa shughuli muhimu kwa kuingiza Uchumi wa watu wa pangani pamoja na kuwa chanzo muhimu cha kuingizia mapato halmashauri ya wilaya ya Pangani.