Pangani FM

Mapishi ya mazoea yakwamisha juhudi za serikali kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia

14 November 2025, 21:46

Picha ikionesha upishi kupitia jiko la kuni, maeneo ya vijijini: Picha mtandaoni

Na Catherine Sekibaha

Makala hii ya Nitunze Nikutunze inaangazia namna mazoea yaliyojengeka kwenye jamii ya watu wengi kwamba ili chakula kiwe kizuri ni lazima kipikwe na nishati isiyo safi ilhali nishati hiyo si rafiki kwa mazingira wala kwa afya zao

Ambapo kupitia changamoto wanazokumbana nazo wanawake katika mapishi Raisi Samia Suluhu Hassan ametilia mkazo suala la watu kuhamia kwenye matumizi ya Nishati safi ya kupikia kupitia kampeni alizoanzisha mijini na vijijini ili kuwanusuru wanawake na adha za kiafya na kimazingira.

Kupitia makala hii utasikiliza namna ambavyo wananchi wanahamia taratibu kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo nimekutana pia na wakinamama ambao wanatumia nishati safi ya kupikia na pia nimezungumza na wakinamama wanaopika chakula kimazoea

Karibu kusikiliza hapa