Pangani FM
Pangani FM
5 August 2026, 20:59

Wazazi wa toto huyu wameonesha mfano wa ushirikiano mkubwa sana kwetu, na hii inaonyesha kwamba jamii tukishirikiana na wataalamu wa afya basi tunaweza kupata matokeo naiomba jamii iiamini hospitali yao kwa sasa ina uwezo wa kufanya mambo kama haya. Amesema Dokta Hasan Msafiri Mgangaa wa hospitali ya wilaya ya Pangani.
Na Saa Zumo
Hospitali ya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga imeandika historia kwa kuwakabidhi wazazi mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati, baada ya kufanikiwa kuokoa maisha yake kupitia huduma za wodi maalumu ya watoto wachanga na watoto njiti (NICU).
Mtoto huyo alizaliwa Juni 11, 2026 akiwa na uzito wa gramu 900, baadaye akashuka hadi gramu 800 kutokana na changamoto za ukuaji. Baada ya kupatiwa huduma kwa takribani miezi miwili, leo ameruhusiwa kurejea nyumbani akiwa na uzito wa kilo 1.63.
Taarifa yake SAA ZUMO inatuarifu kwa kina…