Pangani FM

Mradi wa maji matamu kutilia mkazo Kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani

9 January 2026, 13:10

Picha ya tanki la maji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 katika kijiji cha Boza wilayani Pangani

Na Catherine Sekibaha

Makala hii inazungumzia mradi wa miji 28 unaotarajiwa kutoa maji baridi yaani yasiyo na chumvi ambao umejumuisha wilaya ya Pangani, Muheza, Korogwe na Handeni ambapo unakwenda kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji.

Mradi huo unatarajiwa kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa kutoa huduma ya maji ya uhakika kwa masaa 24 ambayo yanatoka kwenye Mto Pangani hali ambayo itakwenda kutilia mkazo kauli mbiu ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani na pia kuburudisha mioyo ya wananchi kwa kukata kiu yao kupitia maji matamu.

Ambapo awali wananchi wakiwa na uhitaji wa maji baridi yani yasiyo na chumvi walikuwa wanasubiri mpaka mvua inyeshe au waagize maji hayo kutoka Tanga mjini.