Pangani FM

Safari ya miaka 13 ya Pangani FM yawavutia wadau

8 August 2024, 17:39

Picha ya pamoja wafanyakazi wa Pangani FM na mwezeshaji wa jukwaa la mtandaoni Tadio Amua Rushita baada ya kikao cha mafunzo ya kuchapisha habari katika jukwaa la Tadio.

Pangani FM ilianza kurusha matangazo yake rasmi tarehe 08 Agosti 2011 ikiwezesha jamii katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ikitumika kama daraja kati ya wanajamii na viongozi wao.

Na Kokutona Banyikila

Ikiwa leo kituo cha matangazo cha Pangani FM Radio kinatimiza miaka 13 tangu kuanzishwa kwake, watendaji wa kituo hicho washauriwa kuendelea kuzalisha maudhui yenye kuelimisha na kuleta chachu ya mabadiliko kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Zahoro Ramadhani mkuu wa gereza Pangani na ameeleza kuwa maudhui ya Pangani FM radio yanakidhi matakwa ya jamii.

Sauti ya Zahoro Ramadhani mkuu wa Gereza Pangani

Naye afisa uhamiaji wilayani Pangani Bi. Jenester Nitapula ametoa pongezi kwa Pangani FM radio na kuwashauri kuzalisha filamu zitakazosaidia kujitangaza.

Sauti ya afisa uhamiaji wilayani Pangani Bi. Jenester Nitapula

Kwaupande wa mtendaji kata ya Mkwaja Khamis Masoud ameelezea kituo hicho kilivyofanikiwa kuwa karibu na wananchi na kujenga uaminifu wa kupata taarifa kwa urahisi.

Sauti ya mtendaji kata ya Mkwaja Khamis Masoud

Shekhe mkuu wilayani Pangani Zuberi Nondo ametoa matamanio yake kwa Pangani FM Radio kumiliki kituo cha television.

Sauti ya Shekhe Mkuu wilayani Pangani Zuberi Nondo

Pangani FM inarusha matangazo yake kupitia masafa ya 107.5 ikisikika ndani ya mkoa wa Tanga pia ikipatikana dunia nzima kupitia www.radio.tadio.co.tz/panganifm.

Happy birthday 107.5 Pangani FM Sauti ya jamii