Pangani FM
Pangani FM
11 May 2026, 12:27

“Kuanzishwa kwa wodi maalumu ya uangalizi wa watoto wachanga na watoto njiti (NIKU) katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, umeongeza upatikanaji wa huduma za karibu na kwa wakati kwa watoto wanaohitaji uangalizi maalumu”
Na Saa Zumo
Hospitali ya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga ni moja kati ya Hospitali Kongwe hapa nchini ina Zaidi ya miaka 60 na tangu kuanzishwa kwake haikuwepo Wodi maalumu ya uangalizi wa watoto wachanga na watoto njiti (NIKU) jambo lililochangia watoto wanaozaliwa na changamoto za Upumuaji, Manjano, Moyo, Watoto njiti na wa Magonjwa mengine walikuwa wakipewa Rufaa kuelekea hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo jambo lilichangia vifo vya watoto hao ambao walikuwa wakitokea maeneo mbali mbali ya wilaya ya Pangani.

Kuanzishwa kwa wodi maalumu ya uangalizi wa watoto wachanga na watoto njiti (NIKU) katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, umeongeza upatikanaji wa huduma za karibu na kwa wakati kwa watoto wanaohitaji uangalizi maalumu.
Huduma hizo zimechangia kuboresha afya za watoto wachanga na kupunguza vifo vinavyotokana na kuzaliwa njiti au matatizo yanayotokea mara baada ya kuzaliwa.
Mwandishi wetu Saa Zumo ameandaa makala ifuatayo Bonyeza hapa kusikiliza hapa