Pangani FM
Pangani FM
25 July 2025, 20:55

Na Cosmas Clement
Suala la uhifadhi wa misitu huhitaji ushirikiano na jitihada kubwa kuhakikisha hakuna muingiliano wa shughuli za kijamii ndani yake ikiwemo ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia pia kwa ajili ya kukata magogo ya mbao.
Katika kijiji cha Mtonga kilichopo wilya ya Pangani wameamua kuanzisha njia ya ufugaji nyuki katika misitu ya kijiji hicho ambayo ilikuwa ikishambuliwa na baadhi ya wanajamii ambao siyo waamini.
Njia hii imeonekana kuleta mabadiliko katika uhifadhi wa misitu tofauti na awali ambapo vyanzo vya maji vya asili vimeanza krudi katika hali yake ya kawaida.