Pangani FM

Halmashauri ya Pangani kugawa miche 544,000 ya Mkonge.

7 June 2022, 1:46 pm

Halmashauri ya wilaya ya Pangani mkoani Tanga kupitia idara ya Kilimo imefanikiwa kukuza miche 544,000 ya zao la Mkonge.

Akizungumza katika mahojiano na Pangani FM leo Afisa kilimo wa Halmashauri hiyo Bw. Ramadhani Zuberi amesema miche hiyo imekuzwa katika vitalu vinne tofauti vilivyopo katika vijiji vya Msaraza, Jaira,Masaika na Mbulizaga.

Afisa huyo ameeleza kuwa wanategemea kuigawa miche hiyo ifikapo mwezi wa 8 mwaka huu hivyo wakulima wafanye maadalizi ya mashamba pamja na kutoa taarifa kwa idara.

Utekelezaji huo unatokana na agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa alilotoa wakati wa ziara yake Mkoani Tanga ambapo alizitaka Halmashauri zote kuandaa vitalu vya mbegu za Mkonge na kuzigawa kwa wakulima.

Ukuzaji huo wa miche umegharimu zaidi ya Shilingi Mil 30.