Pangani FM

Jela miaka 20 kwa kuwadhalilisha kingono watoto Pangani.

28 March 2022, 4:14 pm

Mahakama ya wilaya Pangani imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela Sideti Itekno baada ya  kupatikana na shataka la  kufanya udhalilishaji  wa kingono.

Katika hati ya mashtaka iliyowasilishwa na polisi mahakamani hapo ilidaiwa kuwa mnamo tarehe 7 mwezi wa 2 mwaka huu ndani ya wilaya ya Pangani,mshtakiwa huyo aliwadhalilisha kingono watoto wa kike wawili wote wakiwa na umri wa miaka 3,na baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili mahakama ilimkuta na hatia hivyo kiuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 23 mwezi wa Machi  mwaka huu na Hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya wilaya ya Pangani Mheshimiwa Joel Mnguto.