Pangani FM

Majeruhi ajali ya Saadani wapokelewa Pangani.

22 February 2022, 7:13 pm

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Dkt. HASSANI MSAFIRI amesema Majeruhi Wawili katika Ajali iliyotokea Jana maeneo ya SAADANI wamepewa Rufaa ya kwenda Hospitali ya Mkoa BOMBO na wengine bado wanaendelea kupatiwa Matibabu Hospitalini hapo.

Akizungumza na Kituo hiki kwa Njia ya SIMU Dkt. HASSANI amesema mpaka wanafika eneo la Tukio walikuta Idadi ya Majeruhi wapatao 23, ambao walianza kupatiwa huduma ya kwanza kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Pangani.

Kwa Mujibu wa Taarifa Gari iliyopata Ajali ilikuwa imewabeba watu waliokuwa wanakwenda Msibani kuzika.