Pangani FM

Ajinyonga kisa wivu wa mapenzi Pangani.

18 August 2021, 1:30 pm

Kijana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Amury Mwin-dadi mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Kijiji cha Mikinguni Wilayani Pangani Mkoani Tanga ajinyonga kutokana na wivu wa kimapenzi.

Mrakibu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Pangani ASP ELIJAH MATIBU amethibitisha kisa hicho kwa kusema kuwa uchunguzi wa awali umebainisha kuwa kijana huyo ambaye ni Bobadoba amejinyonga kutokana na wivu wa mapenzi.

Hata hivyo mwili wa Kijana huyo tayari umezikwa hapo jana kijijini kwao MIKINGUNI.