Pangani FM

Mikononi mwa Polisi kwa tuhuma za kumbaka Binti wa Miaka 6.

10 January 2021, 2:06 pm

Jeshi la Polisi wilayani Pangani mkoani Tanga linamshikilia kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Ramadhani Omari mwenye umri wa miaka 25 Mkazi wa Wilaya ya Pangani kwa tuhuma za kumbaka binti mdogo wa miaka sita.

Akizungumza na Pangani FM ofisini kwake Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Pangani ASP ELIJA MATIKU amesema kuwa kijana huyo alimuingiza ndani kwake binti huyo ili  kutekeleza kitendo hicho.

Kwa mujibu wa Jeshi hilo tayari Madaktari wamethibitisha kuwa Binti huyo ameingiliwa.

Aidha ameeleza kuwa kijana huyo amekamatwa katika kijiji cha Sakura  akiwa anakimbia kuelekea Mkata wilayani Handeni,  kupitia kijiji cha Mkaramo kwa kutumia usafiri wa Pikipiki.

Baada ya Jeshi hilo kupata taarifa liliweka mtego uliofanikisha kumnasa kijana huyo majira ya saa 6 Usiku.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu baada ya hatua za awali za upelelezi kukamilika.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Matiku ametoa wito kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao na kufuatilia nyendo za watoto wao, na kwa vijana na wanaume watu wazima kuacha kufuatilia watoto wadogo.