Pangani FM

TARURA kuufungua mji wa Pangani kwa barabara za lami

6 October 2023, 1:34 pm

Meneja wa TARURA wilaya ya Pangani Mhandisi Elia Mgaya.

Ukimulika nyoka unaanzia miguuni, kwahiyo tumeanza kujenga barabara za mjini kisha tutaenda kujenga za vijijini.

Na Maajabu Ally.

Uongozi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA wilaya ya Pangani mkoani Tanga umesema unaendelea kuufungua mji huo kwa kujenga miundombinu ya Barabara kwa kiwango cha lami.

Hayo yamezungumzwa Octoba 6, 2023 a Meneja wa TARURA wa wilaya hiyo Mhandisi Elia Mgaya wakati akiongea na Pangani FM kwenye kipindi cha Asubuhi ya Leo.

Sauti ya meneja wa TARURA wilaya ya Pangani Eng. Eliya Mgaya.

Katika hatua nyingine amewataka Wananchi kuacha tabia ya kutupa uchafu ovyo kwenye mitaro mikubwa iliyo pembezoni mwa barabara ili kuzuia mitaro hiyo kujaa maji wakati wa msimu wa mvua.

sauti ya meneja wa TARURA wilaya ya Pangani.

Pia ameisisitizia suala la jamii kuendelea kufanya usafi kwenye miundombinu hiyo na kulinda miundombinu ya Barabara kwa maendeleo ya uchumi na taifa kwa ujumla.

Sauti ya meneja TARURA wilaya ya Pangani.

Tangu kuanziashwa wakala huyo mji wa Pangani umeshuhudia ongezeko la ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami kila mwaka.