Pangani FM
Pangani FM
12 June 2026, 14:29

Na Hamisi Makungu
Kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa Wilaya ya Pangani juu ya ukosefu wa maji safi na salama licha ya kuishi karibu na mto Pangani, kilisikika zaidi katika Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambacho kiliwasilishwa na Mbunge wao Mhe. Jumaa Hamidu Aweso.
Mara kwa mara Mhe. Aweso aliuliza Serikali uwezekano wa kutumia mto Pangani ambao unatiririsha maji baharini kutatua changamoto ya maji katika wilaya ya Pangani na Wilaya za Jirani.
Miaka imepita, hatimae kilio hicho sasa kinakwenda kupatiwa ufumbuzi chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan kupitia Mradi wa Maji Miji 28, huku Mbunge wa Pangani akiwa ndie Waziri wa Maji Nchini Tanzania.
Mwandishi wetu Hamisi Makungu ameimulika safari hii ya Waziri wa Maji katikati ya ndoto iliyokuwa na Matumaini na sasa inakwenda kutimia.